Maandalizi Ya Michezo Ya Maigizo Ya Redio Deutsche Welle Idhaa Ya Kiswahili Kwa Msimu Mpya 2017 -2018 “Noa Bongo Jenga Maisha Yako “Yalioanza May 9 ,2017 Yamehitimishwa Leo Kwa Mafanikio Makubwa.



Idhaa ya kiswahili ya Redio Deutsche Welle kupitia timu yake ya uandaaji wa  kipindi cha “Noa Bongo Jenga maisha yako” leo wamefanikiwa kukamilisha maandalizi ya michezo ya kuigiza ya redio kwa lugha fasaha ya kiswahili katika studio za Aegis zilizopo  Kawe Jijini Dar e s salaam.
Katika kuhitimisha kazi hiyo, Timu ya "Noa Bongo" ilipewa nguvu na Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili, Bi Andrea Schmidt Ambaye amefika nchini Tanzania kwa ajili ya kuhakikisha kazi hiyo inakamilika kama ilivyokusudiwa pamoja na kuwapa moyo watendaji Kazi ya uigizaji wa sauti wa  michezo hii ya redio.
Ambapo kwa kiasi kikubwa  Bi Andrea, amefurahishwa na kazi  iliyofanyika ikisimamiwa vizuri na Grace Patricia Kabogo ambaye ni  Mtangazaji kutoka Dw  Ujerumani Pamoja na Michael Springer
Aidha mchezo unaoendelea Kurekodiwa ni muendelezo wa hadithi ya “Karandinga”.
Wa kwanza Kutoka kulia ni Technician  Wa sauti kutoka Dw Mr Michael Springer  , Wa pili kutoka kushoto ni Mr.Ahmed Simba Mkurugenzi wa Dar journalism Academy  Alipotembelea studio hizo mapema hii leo  akifuatiwa na Grace kabogo Dw na kulia kwake Grace ni Mkuu wa Idhaa ya kiswahili Bi.Andrea Schmidt


Rachel Kubo kutoka kulia, Simion John Katikati,Na kushoto ni  Aloyce Michael

Grace Patricia Kabogo -Mtangazaji DW  Ujerumani




Rachel Kubo katikati , kulia  ni  Aloyce Michael na kushoto ni  Mzome wa Mzome wote ni waigizaji wa sauti katika Michezo ya kuigiza inayorushwa na DW




   
 Picha na. Nechi Makundi
Share on Google Plus

About djamultimediaproduction

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni:

Chapisha Maoni