Nyemo Fm Redio 97. 7 Mbiu Ya Dodoma Sports Bonanza 2017 | Na Chuo Cha MiPango

Asubuhi na Mapema Maandalizi Yakifanyika Katika viwanja vya Maisha Plus Dodoma 








Nyemo Fm Redio 97. 7 Mbiu Ya Dodoma, imeanzisha Bonanza Maalum La Michezo Kwa Ajili Ya Kuhamasisha Jamii Kufanya Mazoezi Ya Viungo.

Bonanza Hilo lenye Mwendelezo Kwa Vyuo Vyote Vilivyopo Mjini Dodoma lina lengo la  Kuwaunganisha wanafunzi /Wananchi mmoja moja kwa nafasi yake na redio yao pendwa  Nyemo Fm Ikiwa ni  pamoja na  Kufanya Mazoezi Ili Kuimarisha Afya Na Kujenga Mahusino Baina Ya Familia,Taasisi Na Mashirika Mbalimbali Hapa Nchini.

Jengo la Nyemo Fm Radio 97.7 Dodoma
Akifungua Bonanza Hilo La Kwanza Lilifanyika Chuo Cha Mipango, Mkurugenzi Wa Manispaa Ya Dodoma Godwin Kunambi Amesema Serikali Inaipongeza Nyemo Fm Redio Na inawaomba Kwenda Mbali Zaidi Hasa Wilayani Ili Kuweka Wigo Mpana Wa Mahusiano Kupitia Michezo.
General Manager Nyemo FM  Mr.Elia Mosha Akisaidiana na vijana kufanya Maandalizi ya bonanza

'' Jamani Tuseme Tu Jambo Hili Ni Jambo Zuri Hasa Kwa Sisi Vijana, Lakini Hata Kwa Wasio Vijana. Nyemo Fm Iwe Ni Mfano Wa Kuigwa, Kitendo Hiki Cha Kuanzisha Bonanza Sisi Kama Serikali Kwa Kweli Tunakiunga Mkono Sana Sana Tena Sana, Nawapongeza Sana Nyemo Fm Mmefanya Kitu Ambacho Hakitasahaulika Katika Kumbukumbu Ya Jamii Na Hata Serikali, '' Alisema Kunambi''.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi Mkurugenzi Wa Nyemo Fm Redio, Elia Richard, Alisema Wanafanya Hivyo Ili Kujenga Mahusiano Mazuri Kwa Jamii Lakini Pia Kama Chombo Cha Habari Wanao Wajibu Wa Kutoa Elimu Kwa Katika Masuala Mbalimbali Likiwemo Suala La Michezo.

Alisema Serikali Ya Awamu Ya Tano Kupitia Kampeni Ya Makamu Wa Rais Mama Samia Suluh Hassan, Inawataka Wananchi Kujenga Tabia Ya Kufanya Mazoezi Ya Viungo Hivyo Nyemo Fm Inaunga Mkono Kampeni Hiyo Kwa Kuhamasisha Wananchi Kupitia Mabonanza Kwa Vyuo Vyote Vilivyopo Dodoma.

" Tunaamini Katika Kampeni Hii Kupitia Bonanza, Wanafunzi Watashiki Kwa Wingi Kwa Sababu Wanapenda Michezo na Watatumia Elimu Zao Kuongeza Hamasa Kwa Jamii Kufanya Mazoezi ,” Alisema Richard.
Katika Bonanza Hilo Lililoanzia Chuo Cha Mipango Michezo Mbalimbali Ilichezwa,Ikiwemo Mpira Wa Miguu, Pete,Volleyball, Basketball, Kuvuta Kamba Na Kufukuza Kuku.

Katika Uzinduzi Wa Bonanza Hilo Kwenye Viwanja Vya Maisha Plus Chuo Cha Mipango, Timu Za Mpira Wa Miguu Ziligawanywa Katika Makundi Mawili A Na B.

Mkurugenzi Wa Manispaa Ya Dodoma Godwin Kunambi Akigawa Zawadi
Timu Iliyoingia Katika Hatua Fainali Kutoka Kundi A Ilikuwa Ni Picnic Dhidi Ya Manchester United Kutoka Kundi B Ambapo Katika Fainali Hiyo Timu Ya Picnic Iliibuka Mshindi Kwa Kuifunga Man U Bao 5 - 2 Zilizopatikana Kwa Njia Penati Baada Ya Dakika 30 Kukamilika Bila Kufungana.

Katika Bonanza Hilo Washindi Mbalimbali Wa Kila Mchezo Walipata Zawadi Ambapo Kwenye Mpira Wa Miguu Timu Ya Picnic Ilizawadiwa Mbuzi Mnyama Na Mpira Mmoja, Washindi Katika Mchezo Wa Kuvuta Kamba Wanaume Kwa Wanawake Walizawadiwa Key Holder Na Soda, Kufukuza Kuku Mshindi Mwanaume Na Mwanamke Walizawadiwa Kuku Na Key Holder.

Timu Zingine Zilizopata Zawadi Ni Timu Ya Volleyball Kutoka Mipango Ambao Walizawadiwa Mpira Na Timu Ya Basketball Pia Kutoka Mipango Nayo Ilipata Zawadi Ya Mpira.







General Manager kushoto Mr.Elia Mosha na Mgeni wake Bw. Martin Richard aliyefika kumpiga tafu

Team ya Nyemo iliyopambana kufanikisha Bonanza













Mr. Eric  Kutoka  #TECNO MOBILE TANZANIA Kushoto Na General Manager Nyemo Fm Mr.Elia Mosha
















Share on Google Plus

About djamultimediaproduction

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 maoni:

Chapisha Maoni